Wakaazi wavunja ukuta uliojengwa kuzunguka eneo ambalo wanadai ulinyakuliwa Nakuru
24th June, 2015
Siku chache baada ya wakazi wa eneo moja la Nakuru kupinga unyakuzi wa ardhi yao, zogo jengine limeibuka leo katika mtaa mmoja wa Nakuru. Wakaazi wa Rhonda waliojawa na ghadhabu walivamia na kuvunja ukuta uliojengwa kuzunguka eneo ambalo wenyeji wanadai ni mahala palipotengewa upanuzi wa barabara.