Bingwa wa Olimpiki Mo Farah ajitetea kuwa hajawahi tumia dawa za kusisimua misuli.
19th June, 2015
Bingwa wa Olimpiki kwa mita 5000 na elfu kumi, Mo Farah wa Uingereza, amejitetea kuwa hajawahi tumia dawa za kusisimua misuli. Farah, ambaye ripoti ilifichua jana kuwa alikosa kufanyiwa uchunguzi kabla ya mashindano ya Olimpiki ya London mwaka wa 2012, alisema kuwa madai ya kumuhusisha na matumizi ya dawa hayana ukweli wowote.