Familia ya Falvious Owino yaomba dada yao afungwe nchini Kenya badala ya kunyongwa Uchina
16th May, 2015
Familia ya mwanamke wa umri wa miaka 28 aliyehukumiwa kunyongwa nchini Uchina sasa imetoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili dada yao afungwe nchini Kenya. Familia hiyo imeteta kuwa haikujulishwa mapema kuwa Falvious Owino alikuwa ametiwa nguvuni nchini Uchina.