Maskwota wa Mombasa wafurushwa na maafisa wa polisi katika shamba
10th May, 2015
Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 16 mjini Mombasa, amelazwa katika hospitali kuu ya pwani akiuguza jeraha la risasi mguuni. Alipata jeraha hilo kufuatia utata wa ardhi ambapo baadhi ya Maskwota katika eneo la utange waliandamana kupinga wasifurushwe na nyumba zao zisibomolewe hali iliyosababisha polisi kuwatawanya.