Mshukiwa wa ugaidi mahakamani baada ya kupatikana karibu na shamba la kifamilia ya rais Uhuru
22nd April, 2015
Mshukiwa wa ugaidi amefikishwa mahakamani hii leo baada ya kupatikana karibu na shamba la kifamilia la rais Uhuru Kenyatta. Said Mire Siyad alikamatwa na maafisa wa kupambana na ugaidi huku mahakama ikiwapa polisi siku kumi na tano kufanya uchunguzi zaidi kumhusu.