Eugene Wamalwa ateuliwa waziri huku Francis Kimemmia akitemwa kufuatia mabadiliko serikalini
17th April, 2015
Rais Uhuru Kenyatta,amefanya mabadiliko serikalini jioni hii na kuwateua viongozi wa asasi mbali huku wengine wakistaafu na baadhi wakiondolewa.
Rais Kenyatta ameteua jenerali Samson Mwathethe kuwa mkuu wa majeshi ya Kenya, akichukua nafasi ya jenerali Julius Karangi ambaye amestaafu sasa. Jenerali Mwathethe alikuwa mkuu wa jeshi la wanamaji na vilevile naibu mkuu wa majeshi.