Wanakijiji wa Butere waomboleza kifo cha afisa wa polisi aliyeuawa katika shambulizi la Garissa
4th April, 2015
Huku familia zikiendelea kuomboleza vifo vya wanafunzi waliofariki huko Garissa, familia moja kutoka mjini Butere pia imepatwa na msiba baada ya kijana wao Peter Masinde ambaye ni afisa wa polisi wa Utawala aliyefika katika chuo cha Garissa kuwanusuru wanafunzi hao pia kuuawa katika shambulizi hilo.