Mazungumzo baina ya serikali na Waitiki yatazaa matunda,asema Charity Ngilu
18th March, 2015
Waziri wa ardhi Charity Ngilu amehakikishia wenyeji wa kaunti ya Mombasa kwamba mazungumzo baina ya serikali na mmiliki wa shamba linalozozaniwa la Waitiki yatazaa matunda hivi karibuni.Ngilu amewarai wenyeji kuwa na subra ili kuiruhusu serikali kutafuta mbinu mwafaka ya kusuluhisha utata uliopo.Ngilu amekanusha madai yaliyopo kwamba afisi yake haijakuwa ikiwasiliana na waitiki.