Bei ya mafuta yapanda kwa Sh4 na senti sabini na tano
14th March, 2015
Bei ya mafuta ya mwezi machi 14 hadi Aprili 14 imepanda. Kulingana na bei mpya iliyotolewa na tume ya kawi nchini bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa shilingi 4.75 hadi shilingi 89.46 huku ile ya mafuta aina ya Diesel ikipanda kwa senti 68 hadi shilingi 76.20 na mafuta taa yakipanda kwa shilingi 3 hadi shilingi 55.