Mashindano ya Tennis ya wachezaji walio na ulemavu yalikamilika hii leo Jijini
1st March, 2015
Mashindano ya Tennis ya wachezaji walio na ulemavu yalikamilika hii leo Jijini Nairobi huku wachezaji wa Afrika Kusini wakidhihirisha ubabe wao katika fainali. Els Leon alimlaza Etalli Ayoub kutoka Morroco katika upande wa wanaume huku Venter mariska Akimlaza El Houry Azhour kutoka Morroco katika fainali za kina dada.