Tume ya ardhi yarejesha ekari 45 ya ardhi iliyokuwa imenyakuliwa mjini Eldoret
25th February, 2015
Tume ya ardhi imebatilisha stakabadhi ghushi za ardhi na kurejesha ekari 45 ya ardhi iliyokuwa imenyakuliwa mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu.
Ardhi hiyo ambayo ilikuwa inazozaniwa baina ya kanisa la katoliki la eldoret na serikali ya kaunti ya uasin gishu imerejeshwa kwa serikali ya kaunti hiyo. Mwenyekiti wa tume ya ardhi nchini Mohammed Swazuri sasa ameikabidhi serikali ya kaunti hiyo stakabadhi za umiliki wa ardhi hiyo. Swazuri ametamaushwa na jinsi makanisa yanavyojihusisha na unyakuzi wa ardhi na kuwataka viongozi wa kanisa kujiepusha na dhana hiyo ya unyakuzi.