Mwekezaji wa kibinafsi Ashok Shah akana madai ya kutaka kumuangamiza mbunge Simba Arati
11th February, 2015
Mwekezaji wa kibinafsi Ashok Shah anayedai kumiliki kipande cha ekari 7 mtaani Lavington ambaye mbunge wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati alidai kutaka kumwangamiza amejitokeza na kukana madai hayo. Ashok Shah anasema kuwa mbunge huyo anajaribu kucheza karata ya kisiasa kwani amewahi kuripoti tofauti zao kwa polisi zaidi ya mara tatu.