Kenya halisi: Wanabendi wa Less Kilimabongo wamekufa na kusalia mmoja tu Francis Danger
25th January, 2015
Vibao kama Kenya Nchi Yangu ..Hesabu Gharama na vingine vya bendi ya Less Kilimabongo huenda visiishe ladha leo wala kesho tangu miaka ya sabini vilipotungwa. Lakini je, wafahamu kuwa wanabendi hao wamekufa na kusalia mmoja tu? .Lofty Matambo alipatana naye mtunzi Francis Danger kutoka Kangundo anayekiri kuishi maisha yasiyowiana na sifa walizokuwa nazo.