Geoffrey Kamwororo aibuka mshindi wa mbio za nyika
24th January, 2015
Geofrey Kamworor na Stacey ndiwa ndio washindi wa mbio za nyika za idara ya polisi zilizoandaliwa ngong race course Jumamosi asubuhi. Geoffrey Kamworor alimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika 37 sekunde 23. Stacy ndiwa aliwapiku wenzake akiwemo bingwa wa mbio za mita 10,000 vivian cheruiyot na kuibuka mshindi upande wa kina dada.