Mtoto wa muuzaji wa mnazi apata alama ya 423 kwenye KCPE
9th January, 2015
Kufutiliwa mbali kwa mfumo wa kuwaorodhesha wanafunzi bora nchini huenda kuliondoa mihemko inayohusishwa na mitihani ya taifa......lakini katika mtaa mmoja wa mabanda eneo la Changamwe mombasa bado sherehe za mtoto wa muuzaji mmoja wa mnazi zinaendelea…. Kijana huyo alijikusanyia alama zaidi ya 420 licha ya ufukura unaodhirika nyumbani kwao.....