Viongozi wa makanisa wametoa wito kwa Rais Uhuru kubaini palipo na pengo kwa idara ya usalama
26th November, 2014
Miungano ya makanisa ikiwemo NCCK na makamishna wa haki na amani katika tume ya makasisi katika kanisa la katoliki kote nchini wamezidi kuishinikiza serikali kushughulikia kwa haraka iwezekanavyo suala ya usalama wa kitaifa, kufuatia visa vya ukosefu wa usalama vinavyoendelea kushuhudiwa humu nchini. Viongozi hao wametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kubaini palipo na pengo katika idara ya usalama wakidai kuwa ni dhahiri kuna ukosefu wa uratibu baina ya maafisa wa usalama na rasilmali.