Mhubiri Victor Kanyari aendelea kutengwa na mashirika ya kidini
10th November, 2014
Mhubiri Victor Kanyari anayekabiliwa na tuhuma za utapeli ameendelea kutengwa na mashirika ya kidini tangu KTN kufichua shuguli zake . Na leo baraza la makanisa nchini NCCK limeunga mkono hatua ya mwanasheria mkuu ya kutoa nafasi ya kuandaliwa kwa sheria za kusimamia utendakazi wa makanisa nchini.