Wazazi wapokea vyema mapendekezo ya kupunguza gharama ya elimu ya sekondari
30th October, 2014
Mapendekezo ya kupunguza gharama ya elimu ya sekondari, bila shaka yanapokelewa vyema na wazazi. Lakini je yanaenda sawia na uhalisia wa kumudu elimu ya sekondari? Je yataboresha au yataporomosha viwango vya elimu? Ni baadhi tu ya maswali yaliyoibuka kwenye mkutano wa John Juma na mwalimu mkuu wa shule ya kitaifa ya Shimo la Tewa mjini Mombasa.