Mtu mmoja anayeshukiwa kumnajisi mwanawe atiwa nguvuni huku wazee wakimtetea asikamatwe
12th October, 2014
Mtu mmoja anayeshukiwa kumnajisi mwanaye hatimaye alitiwa nguvuni hii leo eneo la Lurambi kaunti ya Kakamega. Wakazi walimnasa na kumkaripia vikali baada ya masaa mawili alipokuwa amechana mbuga. Lakini kama anavyoripoti mwanahabari Francis Ontomwa, baadhi ya wazee walikashifu mkondo huu wakitaka kutatua maswala haya pasi na kuwaalika maafisa wa kulinda usalama.