Wenyeji wa eneo moja katika Kaunti ya Isiolo wangali wanategemea barua ya posta kuwasiliana
3rd October, 2014
Ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano nchini, umewafanya wakenya wengi kujiunga na tabaka la kuwasiliana kwa njia ya mitandao ya twitter, facebook na teknolojia ya video ya skype. Lakini katika eneo moja la kaunti ya isiolo wenyeji wangali wanategemea barua ya posta kuwasiliana kwa kuwa ugumu wanaopata wakitaka kupiga simu ni wa kutatiza. Kwanza lazima mtu apande tanki moja la maji lenye kimo cha mita kumi na tano ndipo simu yake iweze kupokea na kupiga. Hali hii ni changamoto kuu kwa wanawake. Carol nderi amerejea kutoka isiolo kusini na hapa anasimulia.