Maafisa wa riadha tawi la Uasin Gishu wamuonya Isaiah Kiplagat dhidi ya kuingilia mipangilio yao
30th September, 2014
Maafisa wa riadha tawi la Uasin Gishu wamemkosoa mwenyekiti wa kitaifa, Isaiah Kiplagat na wamemuonya dhidi ya kuingilia kati mipangilio zao. Wakiongozwa na mwenyekiti wao Benjamin Limo, maafisa hao wanasema hatawafanya kazi na mwenyekiti wa tawi la nandi, Abraham Kimutai. Kimutai alipoteza kura dhidi ya Wilfred Bungei lakini inadaiwa mwenyekiti Kiplagat alitupilia mbali matokeo ya zoezi hilo.