David Kimaiyo aamuru maafisa wote wanaotumia silaha zao kiholela kufunguliwa mashtaka
24th September, 2014
Inspekta generali David Kimaiyo amewatahadharisha maafisa dhidi ya kutumia silaha zao kiholela na kusababisha maafa na majeraha kwa watu. Kimaiyo amesisitiza kuwa sheria hairuhusu upigaji risasi washukiwa kwa kusudi la kuua ila tu pasipo budi. Ameamuru maafisa waliofyatua risasi katika kisa cha makueni kukamatwa na wafunguliwe mashtaka. John Juma anaripoti