Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Nairobi wazua rabsha kwa kuchelewa kwa fedha za HELB
19th September, 2014
Barabara zilizoko karibu na Chuo kikuu cha Nairobi hii leo zilifungwa kwa muda na wanafunzi waliozua rabsha. Wanafunzi hao wa chuo kikuu cha Nairobi walikimbizana na maafisa wa polisi kwa muda kwa kile wanachosema ni kuchelewa kutolewa kwa mikopo yao ya masomo maarufu kama HELB . Anavyoarifu Agnes Penda, wanafunzi wa Chuo cha Mombasa Technical, vilvile walizua fujo mjini Mombasa.