Mwanamke mmoja Limuru ajitolea kuwatengezea wasichana Visodo vya Hedhi
13th September, 2014
Kulingana na utafiti wa UNESCO, mmoja kati ya wasichana kumi hukosa shule kwa sababu ya hedhi na baadaye kuacha shule. Wengi wametumia vitambaa wakati huu ambavyo vina uwezo wa kuwasabishia magonjwa. Lakini mwanamke mmoja huko Limuru amejitolea kuwasaidia wasichana kama hao haswa wasio na uwezo wa kupata Visodo vya Kisasa.