Polisi watia nguvuni jamaa watatu waliokuwa wakijifanya kuwa Maafisa wa Polisi
9th September, 2014
Jamaa watatu wanaodaiwa kuhangaisha wenyeji kwa kujifanya kuwa maafisa wa polisi katika eneo la Kivumbini mjini Nakuru wametiwa nguvuni. Watatu hao wanadaiwa kuvaa sare za afisa wa polisi na kuwahangaisha raia katika mitaa ya kivumbini, manyani na kaloleni hususan nyakati za usiku.
Naibu wa afisa wa utawala nakuru barnabas kimutai amedai kujuzwa na raia ambao walitamaushwa na jinsi watatu hao walivyokuwa wakiwanyanyasa wenyeji wa eneo hilo . inspekta huyo, amedokeza kuwa polisi wamekuwa wakifanya msako wa wahalifu hao, akidai kuwa mmoja kati ya waliotiwa nguvuni amewahi kuhudumu kama afisa wa polisi. watatu hao wanadaiwa kuwa katika kikundi kijulikanacho kama bongo 4. kwa sasa washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha bondeni mjini nakuru wakisubiri kufanyiwa uchunguzi pamoja na kufunguliwa mashtaka.