Watu kadhaa watiwa nguvuni kwenye msako unaoendelea wa kufunga maabara gushi nchini
6th September, 2014
Bodi ya maabara nchini imefunga takriban kliniki na maabara 50 zinazoendeleza shughuli bila vibali, huku oparesheni hiyo ikiendelezwa katika mitaa mbalimbali hapa jijini. Katika oparesheni ya bodi hiyo maeneo ya Eastleigh na katikati mwa jiji, mojawapo ya kliniki iliyokuwa ikitoa huduma za afya kinyume na sheria ilifungwa huku mmiliki ambaye amejidai daktari ghushi akitupwa korokoroni. Kama anavyoafiru mwanahabri mohamed mahmoud, idadi kubwa ya wakenya walio na mapato madogo hulazimika kutafuta tiba kwa kliniki kama hizi.