Jinsi shughuli ya kuandikisha wafanyikazi kwa mfumo wa elektronoki itakavyofanyika na uzuri wake
1st September, 2014
Huku serikali ikianzisha rasmi shughuli ya kuandikisha wafanyikazi wote wa umma kwa mfumo wa elektroniki ili kuhakikisha kuwa wafanyikazi ghushi wameondolewa, wakenya wanashangazwa na mbinu itakayotumiwa kuhakikisha kuwa ufisadi hautajipenyeza katika shughuli hii. Serikali hupoteza takriban shilingi bilioni 1.8 pesa za umma kila mwaka kupitia kuwalipa wafanyikazi bandia. Mwanahabari mohamed mahmoud anangazia jinsi shughuli hii itakavyofanyika, na uzuri wake katika serikali inayotambulika kama digitali.