Kijana mmoja ametumia ubunifu wake kukarabati studio anayotumia kupeperusha matangazo na nyimbo
17th August, 2014
Kijana mmoja kutoka kaunti ya Bomet ya kati ametumia ubunifu wake kukarabati studio anayotumia kupeperusha matangazo na nyimbo kadha. Kijana nathan kirui mwenye umri wa miaka 25 ameweza kupeperusha matangazo kwa umbali wa kilomita mbili kijijini mwao. Japo hana leseni, anatarajia uzinduzi wake, utampa bahati yakutambulika kote nchini na kupata mfadhili ili akamilishe masomo yake.