Cotu yatishia kuandaa mgomo iwapo Francis Atwoli na Jackline Mugo hawatarejeshewa nyadhifa zao
20th July, 2014
Muungano wa wafanyikazi nchini Cotu umetishia kufanya mgomo wa kitaifa ifikapo tarehe nne mwezi Agosti, wa kushinikiza kurejeshwa kwa katibu wake Francis Atwoli na kiongozi wa chama cha waajiri FKE Jacquiline Mugo,kwenye bodi yaNSSF. Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya cotu, Atwoli amesema kuwa kuna masuala fiche ambayo yanamfanya waziri wa leba kuwaondoa katika bodi ya NSSF, huku akisema kuwa uamuzi wake wa kuandaa mgomo unaungwa mkono na zaidi ya vyama 43 vya wafanyikazi wakiwemo zaidi ya wafanyikazi millioni mbili ambao baadhi yao walifika katika hafla hiyo.