Polisi walazimika kuwatawanya vijana wanaoandamana Majengo, Mombasa
4th April, 2014
Polisi mjini mombasa wamelazimika kufyatua risasi angani na vitoa machozi kuwatawanya vijana waliojaribu kuandamana eneo la majengo dhidi ya kuuawa kwa sheikh abubakar sharrif almaarufu makaburi. Mapema leo polisi walionya dhidi ya maandamano yoyote. Wanaharakati wa kutetea haki za binaadam pia waliahirisha maandamano japo walishutumu polisi kwa hatua hiyo.