Mtoto aliyeibwa na kupelekwa Juba, Sudan Kusini hatimaye arudishwa nchini
21st February, 2014
Maafisa wa Ubalozi wa Kenya na wale wa Sudan kusini wamemrejesha humu nchini mtoto mmoja aliyeibiwa kutoka humu nchini na kupelekwa Sudan Kusini akiwa na umri wa siku nne pekee. Mtoto huyo ambaye amekuwa Sudan Kusini kwa muda wa miezi minne alipokelewa hii leo katika uwanja wa kimataifa wa jkia na maafisa wa serikali huku mshukiwa mmoja akikamatwa kuhusiana na uhalifu huo.