x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Radio Maisha yawaburudisha Mashabiki wa Molo, Nakuru na Naivasha

06, Feb 2014

Maelfu ya mashabiki wa Radio Maisha katika miji ya Naivasha, Nakuru na Molo leo wamepata fursa ya kukutana na msafara wa kituo hicho kinachomilikiwa na shirika la habari la Standard. Msafara huo unaolenga kufika mjini kisumu siku ya jumapili ulifika mjini naivasha ambapo mashabiki wamepewa t-shirts, jezi za kuvaa kwenye pikipiki na zawadi nyengine nyingi. Mashabiki hao wameshindana kunengua nyimbo zilizokuwa zikiporomoshwa na msafara huo na vilevile kujumuika ma wachekeshaji wa kituo hicho zuleka na mshamba . Meneja msimamizi wa Radio Maisha Tom Japanni ambaye anaongoza msafara huo amesema lengo ni kuwapa mashabiki fursa ya kubaini kwamba redio maisha inajali maslahi yao. Mbali na Nakuru, Njoro na Molo msafara huo utaelekea Kisii na Kisumu mwishoni mwa wiki. Msafara huo umeandaliwa kwa ushirikiano na Stima Sacco

RELATED VIDEOS


Feedback