Msichana aliyekuwa amepotea kwa miaka kumi na miwili apatikana
21st December, 2013
Machozi ya furaha yalitanda katika eneo bunge la kibwezi baada ya msichana aliyekuwa amepotea kwa muda wa miaka kumi na miwili kujiunga na familia yake. Jessica Wanza aliye na umri wa miaka kumi na minne alitoweka mwaka 2001 katika mtaa wa kibera hapa jijini. Anastasia Mukiti, ambaye ni dadake msichana huyo anasema wametumia kila mbinu ikiwemo kutumia ushirikina ili kumpata msichana huyo bila mafanikio. Mamake msichana huyo alifariki mwaka 2003. Mwaka huu hata hivyo waliweka tangazo la kupotea kwa mtoto huyo kupitia shirika la kuwasaidia watoto nchini, na baada ya msichana waliokuwa wakimshuku kufanyiwa uchunguzi ikabainika kuwa alikuwa mtoto ambaye wamekuwa wakimtafuta miaka mingi. Jessica alipatikana katika makao ya watoto ya Nanyuki.