Mwanamuziki Tabu Ley Rochereau aga dunia
30th November, 2013
Mmoja wa waanzilishi wa mziki chapa soukus Tabu Ley Rochereau ameaga dunia hii leo. Mwendazake Tabu Ley alifariki akipokea matibabu ya ugonjwa wa kiharusi katika hospitali moja nchini Ubelgiji. Ni mmoja wa wanamuziki watakaoenziwa na kukumbukwa zaidi kupitia miziki yake kama sorozo, maze, sacramento, muzina, miongoni mwazo ambazo alizitunga na kundi lake la Afriza internationale.