×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Zaidi ya watu 900 washikwa mateka katika kijiji cha Lorokon kaunti ya Turkana

23rd November, 2013

Zaidi ya watu 900 wameshikwa mateka nyumbani mwao katika kijiji cha Lorokon kaunti ya turkana baada ya watu wanne waliojihami kwa silaha kuzingira kijiji chao kwa siku 4 sasa. Maafisa wa usalama wameshindwa kufika katika kijiji hicho kutokana na watu zaidi waliojihami kukita kambi katika vituo vya kibiashara vya Kainuk na Nakwamoru ambavyo vimepakana na kijiji hicho. Gavana wa kaunti ya Turkana Josphat Nanok ametoa wito kwa serikali haswa wizara ya usalama kujizatiti katika kuimarisha usalama katika kaunti hiyo haswa Turkana kusini. Akiongea katika afisi yake Nanok amesema visa vya kushambuliwa kwa wananchi na wafanyikazi wa mashirika ya kutoa misaada vimeendelea. Jumatano wiki iliyopita dereva wa shirika la msalaba mwekundu alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi na anapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi huko Eldoret.
.
RELATED VIDEOS