Mwanamke ajikimu kwa magereza
1st November, 2013
Alianza kama seremala wa kawaida, kuchonga fanicha au samani kama vile vitanda, viti na hata kabati na kuwauzia wateja wake. Hata hivyo kazi hii kwake Fatuma Abubakar mkaazi wa eneo la Kaloleni huko Molo haikudumu kwani muda mchache alijipata akiwatengenezea wateja wake majeneza. Fatuma amepitia panda shuka nyingi, kutokana na itikadi kwamba majeneza ni uchinvi wa kukaribisha kifo.