Watu wanne wauawa kufuatia rabsha Mombasa
4th October, 2013
Watu wanne wameuawa na wengine wanauguza majeraha katika hospitali mbali kufuatia rabsha mbaya zilizotanda mjini Mombasa, mchana mzima. Biashara zilifungwa na kila mtu ikiwa kukimbilia maisha yake, pale machafuko yalipochacha kufuatia kuuawa kwa Sheikh Ibrahim na wenzake wanne, jana usiku na watu wasiojulikana.