×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mtoto akatwa mguu hospitalini

2nd October, 2013

Familia moja mjini Nakuru inaishi kwa majonzi baada ya mtoto wao wa kike aliyezaliwa wiki nane zilizopita, kulazimika kukatwa mguu, katika kile wanakitaja kama utepetevu wa madaktari. Salama waithera alizaliwa katika hospitali ya nakuru nursing home, akiwa salama, lakini wiki moja baadaye akashikwa na homa na ndipo wakamrejesha hospitalini humo. Siku mbili baada ya kupewa dawa, wazazi wa salama wakagundua kuwa mguu wake wa kushoto umeanza kuoza na kugeuka rangi isiyo ya kawaida. Alipelekwa katika hospitali ya kijabe, na jumamosi mguu wake ukakatwa. Wasimamizi wa hospitali hiyo hata hivyo wamejitenga na masaibu ya salama, wakisema ugonjwa uliomuathiri wa kufa kwa seli za neva haukusababishwa na dawa walizompa hospitalini humo.
.
RELATED VIDEOS