Khalwale amjadili Ruto na wadhfa wake serikalini
1st July, 2013
Mtazamaji katiba iliyoko sasa inasisitiza kwamba wafanyikazi wa serikali na uongozi wa serikali kwa jumla sharti uzingatie hadhi kama ilivyodokezwa bayana kabisa kwenye sura ya sita ya katiba. Ni kutokana na vipengee hivyo ndiposa Nancy Baraza alichujwa kama naibu jaji mkuu kwa kubainika kuwa alisaliti hadhi aliyopaswa kuwa nayo kama afisaa wa serikakali pale alipomshambulia Rebecca Kerubo, aliyekuwa akihudumu kama bawabu huko village market. Sasa hivi vinywa vya wadadisi vimeanza kuuliza maswali juu ya amri ya mahakama kuu kwa naibu wa rais William Ruto kumlipa Adrian Muteshi shilingi milioni tano na vilevile kumuachia mlalamishi huyo shamba lake ambalo Ruto alimiliki punde tu baada ya Muteshi kuhama huko Uasin Gishu kutokana na machafuko ya mwaka wa 2007. Je, sheria inasemaje juu ya afisaa wa serikali aliyepatikana na hatia mahakamani?