Machifu waachizwa kazi Garissa
26th April, 2013
Huku serikali ikiendelea kuwa ngangari kumaliza mauaji garissa, machifu saba wamesimamishwa kazi, kufuatia msururu wa mauaji katika kaunti hiyo. Hatua dhidi ya machifu hawa inafuatia operesheni kali ilianzishwa mapema wiki hii kuwasaka wahalifu ambao wamekuwa wakisababisha mauaji bila ya hofu, na huku garissa ikiendelea kushuhudia misako, kaunti ya nyeri jamaa ya jamaa ya joseph maina ndung’u ilikuwa inampa buriani. Ndu’ngu alikuwa mmoja wa watu 10 waliouawa katika shambulizi la hivi majuzi garissa.