Serikali yawaonya wanaoeneza chuki kwenye mtandao
15th March, 2013
Serikali imekiri kuwa inakumbwa na changamoto nzito za kudhibiti semi za chuki katika mitandao ya kijamii. Katibu katika wizara ya habari na mawasiliano Bitange Ndemo, amesema baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wa mashirika ya kijamii, wanachukua fursa na kutumia mitandao ya kijamii kusambaza propaganda na semi za uchochezi. Hatahivyo,ndemo anasema kwamba serikali haitatumia njia zilizopitwa na wakati kuwaziba watumizi wa mitandao lakini watawataka watoaji huduma za mitandao kuhakikisha wanatumia anwani maalum kusaidia kuwatambua wahalifu hao.