Kivuitu azikwa Wamunyu, kaunti ya Machakos
10th March, 2013
Aliyekuwa mwenyekiti wa tume iliyobanduliwa ECK Samuel Mutua Kivuitu alizikwa hapo jana katika eneo la Wamunyu kaunti ya Machakos, viongozi waliohudhuria mazishi hayo walimtaja Kivuitu kama msomi na aliyewahamasisha wengi wakati wa uhai wake. Kivuitu aliwahi kusimamia uchaguzi wa 1997, 2002 na ule wa 2007.