×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Kaplana Rawal achaguliwa kuwa naibu Jaji Mkuu

22nd February, 2013

Jaji wa mahakama ya rufaa Kalpana Rawal amependekezwa kuwa naibu jaji mkuu. Rawal aliteuliwa na tume ya huduma za mahakama, JSC baada ya watahiniwa wanne kupigwa msasa. Rawal sasa lakini itabidi asubiri ili kuidhinishwa na bunge lijaalo, kabla ya kuvalia vazi hilo la naibu jaji mkuu rasmi.akitoa tangazo hilo, jaji mkuu willy mutunga alisema walifikia uamuzi wa kumteua rawal kutokana na ujuzi wake wa muda mrefu kuhusiana na masuala ya idara ya mahakama. Rawal alikuwa miongoni mwa watahiniwa watano wa kike waliohojiwa na tume ya huduma za mahakama. Wengine walikuwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wanasheria, raychelle omamo, mwenyekiti wa zamani wa fida Joyce Majiwa, Lucy Kambuni na Profesa Phoebe Nyawade. Wadhifa wa naibu jaji mkuu uliachwa wazi baada ya kujiuzulu kwa nancy barasa. Barasa alijiuzulu baada ya jopo la kumchunguza kuhusiana na kile kisa cha kumdhulumu bawabu rebecca kerubo kuafikia kwamba hafai kuhudumu kama naibu jaji mkuu.
.
RELATED VIDEOS