×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Vikwazo kwa Kenya kuhusu uchaguzi

14th February, 2013

Suala la ICC na uchaguzi mkuu utakaofanyika machi 4, huezi litenganisha na limekuwa kama chanda na pete. Na limetokota zaidi pale semi kutoka mataifa ya magharibi zimetafsiriwa kana kwamba kenya itajipata matatani iwapo ndoto ya uhuru kenyatta na william ruto wanaokabiliwa na mashtaka ya jinai, huko the hague itatimia na kuingia ikulu. Rais wa Marekani Barack Obama, katika ujumbe wa kenya obama alisema marekani haimshabikii mgombeaji yeyote, chaguo la wakenya ni lao wenyewe. Lakini siku kadhaa baadaye balozi wa marekani anayehusika na masuala ya afrika johnnie carson pamoja na mabalozi wa umoja wa ulaya walionekana kugusia kuwa huenda kukawa na athri iwapo kenya itawachagua watu fulani………na ndio mkoko umeanza kualika maua? Je kuna tishio la kenya kuwekewa vikwazo iwapo itawachagua uhuru na ruto?
.
RELATED VIDEOS