News: Afisa auawa na kiboko
1st February, 2013
Afisa mmoja wa kutunza misitu alivamiwa na kuuawa na kiboko usiku wa kuamkia leo eneo la manguo huko nyahururu,alipokua akielekea nyumbani kwake kutoka kazini. Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi nyandarua benjamin onsongo, alisema kwamba afisa huyo alikuwa amemaliza kazi yake mwendo wa saa mbili.