Jamii yadai kitoweo cha punda milia hili wakubali kuhesabiwa
25th August, 2012
Je mtazamaji, ni kitu gani kinachoweza kukushawishi ili uweze kushiriki katika zoezi la kitaifa la kuhesabu watu? Naam, nchini Tanzania, watu kutoka jamii ya kuwinda ya Wahadzabe imeshurutisha serikali ya Tanzania kuwaandalia kitoweo cha nyama ya punda milia ili waweze kushiriki kwenye zoezi la kitaifa la kuhesabu watu linaloanza usiku wa jumapili. Awali, jamii hiyo ilikuwa imependekeza ipewe mlo wa nyani pamoja na pombe kali haramu ijulikanayo kama ‘gongo’ lakini wakuu wa serikali wakadinda. Mwanahabari wetu Patrick Amimo ana mengi.