Sherehe ya kigiriama ya kuwabatiza wageni
11th August, 2012
Kuwa mbali na nyumbani kumewafanya idadi kuu ya raia wa kigeni au hata wakati mwengine watalii eneo la pwani ya Kenya kutaka kujumuika na jamii zinazoishi huko hasa jamii za wamijikenda. Wengi wao wamepata hata kubatizwa majina ya kigiriama hasa katika eneo la Malindi. Mfano mzuri ni mwanasiasa wa magarini Franco Esposito mzaliwa wa Italia ambaye jina lake la kigiriama ni Kasoso wa Baya. Katika sherehe za kumkumbuka mpiganaji wa jamii ya wagiriama Mekatilili wa Menza, sherehe ya kuwapa majina wageni hao haikukosekana na ilitia fora huku watalii wakijitokeza kupokea majina ya kigiriama na mbari za jamii hiyo.