×
× KTN NEWS News Business Sports Politics Features Live Schedule E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Benki ya Co-operative

9th August, 2012

Benki ya Co-operative imenakili ongezeko la asilimia 21.7 ya faida zake katika kipindi cha miezi sita iliyokamilika kabla ya kutozwa ushuru. Kulingana na afisa mkuu wa benki hii Gideon Muriuki, benki hiyo imenakili faida ya shilingi bilioni 4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 3.3 ilizopata katika kipindi sawa na hicho mwaka jana. Kiwango cha mikopo ilichotoa katika kipindi hicho vile vile kimeongezeka kwa asilimia 18.3. Katika kipindi hicho benki hiyo imetoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 112.6. Meneja mkurugenzi wa benki hiyo Gideon Muriuki amesema ongezeko la viwango vya riba katika benki kuu iliathiri utoaji wa mikopo kwa wateja wa benki hiyo katika kipindi hicho.
.
RELATED VIDEOS