Mseto wa kisiasa.
21st July, 2012
Jungu lipo jikoni na kitoweo kitakuwa na utamu si haba. Ndio ujumbe wa eugene wamalwa, moses wetangula na bifwoli wakoli, kwa naibu waziri mkuu musalia mudavadi. Watatu hao ambao wanendeza siasa za kupunguza makali ya mudavadi kuwania urais walipeleka kampeini zao katika nchi jirani ya uganda. Naibu waziri mkuu uhuru kenyatta naye alipiga kambi turkana, huku mudavadi akizuru kisii. Raphael tuju alikuwa mtaani majengo hapa nairobi. Ndio siasa za jumamosi.