Passaris ataka fedha, mali za washukiwa wa ufisadi kuchukuliwa

KTN Mbiu | Wednesday 13 Jun 2018 5:41 pm

Mwakilishi wa kike katika kaunti ya  Nairobi Esther Passaris amevitaka vyombo vya ujasusi  kuzichukua fedha na  mali kutoka kwa wanaoshukiwa kuiba  mali ya umma Passaris amesema kwamba   fedha nyingi zilizoibwa kutoka  kwa idara za serikali kama vile NYS zingesaidia kuleta  maendeleo  mashinani . Passaris aliyekuwa akizungumza katika eneo la Babadogo jijini Nairobi amesema kuwa wafisadi hawafai kuruhusiwa kusherehekea  mali ya umma .